Vipimo
Mchele 2 Vikombe
Tui la nazi zito 2
Vikombe
Hamira 1 Kijiko Cha chai
Unga wa ngano 2 Vijiko
vya supu
Iliki Kiasi upendavyo
Sukari Kiasi upendavyo
Yai 1
Vipimo vya Tui la Kupaka
Tui la nazi 2 Vikombe
Hiliki ya unga Kiasi upendacho
Sukari Kiasi upendacho
Unga wa ngano 1 Kijiko
cha supu
Namna ya Kutayarisha na Kupika
- Changanya vitu vyote vya tui la kupaka katika kisufuria kidogo.
- Lipike tui huku walikoroga mpaka lichemke na liwe zito.
- Osha na loweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
- . Mimina vifaa vyote isipokuwa yai na sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
- . Mimina sukari na yai usage kidogo tu kiasi cha kuchanganya.
- . Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure/uvimbe
- . Ukishafura, weka chuma kipate moto. (Ni bora kutumia kichuma kidogo)
- . Katika sahani ya kupakulia, paka tui kote.
- . Tia kijiko nusu cha chai cha mafuta au samli kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko ukitumia upawa na ufunike.
- . Kibibi kikianza kuiva na kushikana upande mmoja , kigeuze upande wa pili mpaka kigeuke rangi na kuiva.
- . anga kwenye sahani iliyopakwa tui.
- nelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; kila ukiepua kibibi, panga juu ya mwenzake kama ilivyo kwenye picha na upake tui juu yake.
Post a Comment