PILAU YA NG'OMBE NA NYANYA

0 comments


                                             
 
                                                     Vipimo
Mchele 3 vikombe
Nyama ya ngo’mbe 1 kg
Pilipili boga 1 kubwa
Nyanya 2 kubwa
Vitunguu maji 2 vikubwa
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Ndimu 1
Mafuta ya kupikia ½ kikombe
Mdalasini ½ kijiko cha chai
Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ½ Kijiko cha chai
Hiliki ½ Kijiko cha chai
Namna ya kutayarisha na Kupika

 • Roweka mchele wako katika chombo
 • Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi
 • Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya brown
 • katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni
 • Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

 • Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa brown  na tia nyanya
 • Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi
 • Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke
 • Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza
 • Funika na punguza moto na uache uive taratibu
 • Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.Post a Comment