CHAUROO

0 comments

Vipimo
Pawa (pepeta) 1 Kg

Dengu za vipande za manjano 1/2 Kg

Karanga (njugu) zilokiwisha kaangwa ¼ Kg
Korosho ¼ Kg

Zabibu kavu 1 Kikombe

Chips (Crisps plain) 2 Paketi kubwa

Bizari ya manjano 1 kijiko cha chai

Sukari ¼ kikombe

Chumvi Kiasi

Ndimu ya unga 2 vijiko vya chai

Pilipili ya unga 1 kijiko cha supu

Majani ya mchuzi makavu (curry leaves)
(yachambue) Misongo miwili (bunch)
Mafuta 2 vijiko vya supu
Mafute mengine ya kukaangia dengu kiasi
na pepeta katika karai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  • Roweka dengu tokea usiku.
  • Siku ya pili weka mafuta kwenye karai na kwa moto wa kiasi kaanga dengu kisha zitoe.
  • Kisha kaanga pepeta uzito, weka kando.
  • Kaanga zabibu kidogo tu zitoe.
  • Tia mafuta vijiko 2 vya supu katika kikaango (frying pan) kaanga majani ya mchuzi pamoja na bizari ya manjano.
  • Tia kwenye bakuli kubwa vitu vyote ulivyokaanga na uchanganye , pamoja na korosho, njugu na chipsi.
  • Nyunyuzia sukari, ndimu ya unga, chumvi na pili pili ya unga uchanganye vyote pamoja tayari kuliwa.


Post a Comment