0 comments
MAPISHI YA NGURU WA NAZI NA BAMIA
MAHITAJI
Samaki nguru 5 vipande

Thomu na Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagawa kijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi 1 kijiko cha chai

Ndimu 2 kamua maji

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Nguru

Changanya vitu vyote katika kibakuli ufanye masala ya kupaka kwenye samaki.
Roweka kwa muda nusu saa
Paka treya mafuta, kisha mpange nguru na mchome katika oveni.
Atakapoiva upande upande mmoja mgeuze upande wa pili huku unanyunyizia mafuta.
Epua weka kando.Vipimo vya mchuzi


Vitungu maji
Nyanya 2

Tuwi zito la nazi 2 vikombe viwili

Bamia 1 kikombe

bizari ya manjano ¼ kijiko cha chai

Pilipili mbichi 1

Ndimu na chumvi kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Katika sufuria tia tuwi kikombe kimoja, kisha tia bamia ulizokatakata zipike ziwive kidogo.
Saga kitunguu, nyanya na pilipili mbichi katika mashine ya kusagia (blender) kisha mimina katika tui la bamia.
Tia vipande vya nguru, bizari, chumvi, ndimu, kisha tia tui lilobakia.
Acha mchuzi uchemke kidogo kidogo kisha epua utie katika bakuli ukiwa tayari.
(by alhidaya)


Post a Comment