Vipimo
Ndimu / Limau 23
Chumvi 3 Vijiko vya supu
Bizari ya manjano ½ Kijiko cha chai
Pilipili nyekundu nzima ½ Kikombe
Pilipili ya kichina (sambal) 2 Vijiko vya supu
Masala ya unga 1 Kijiko cha supu
Karoti 4
Maji ya ndimu 1 ½ Vikombe
Siki ½ Kikombe
Namna Ya Kutayarisha
- Osha ndimu na ikiwa ni rangi ya kijani unaweza kuchambua maganda, kisha zikate vipande vipande.
- Katika chupa la kiasi, changanya vipimo vyote isipokuwa karoti, maji ya ndimu, siki na sambal (pilipili ya kichina ya chupa).
- Weka chupa pahali pa joto au juani kwa muda wa wiki 2 – 3.
- Halafu ikishaiva ongezea karoti zilizo katwa katwa, maji ya ndimu, siki na sambal na hakikisha mchanganyiko wa maji ya ndimu imefunika ndimu vizuri.
- Na itakuwa tayari kwa kuliwa na wali na venginevyo.
Post a Comment